Walimu
wawili wa Shule ya Msingi Kitarungu wilayani Serengeti wamezipiga ‘kavukavu’
ofisini huku wanafunzi wakishuhudia.
Tukio
hilo limetokea jana Jumatano saa 2.45 asubuhi mwaka na limeripotiwa kituo cha
polisi Mugumu, mkurugenzi mtendaji na serikali ya kijiji hicho.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Thomas Marwa ambaye alijeruhiwa katika ugomvi huo amesema akiwa ofisini akiandaa matokeo ya mtihani alivamiwa na mwalimu Yared Amosi na kumshambulia kwa makonde usoni.
“Kutahamaki
akawa ameishanipiga ngumi tatu usoni na kunijeruhi jicho, nikalazimika kupiga
kelele kuomba msaada," amesema.
Imeelezwa
chanzo cha kushambuliwa ni kufuatia kumbana mwalimu kushindwa kutunga mtihani
wa sayansi kwa darasa la tano, utoro kazini na ameishamwandikia barua ya onyo.
Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Yohana Getari amesema baada ya kusikia kelele alilazimika kukimbilia shuleni na kukuta ugomvi huo na mwalimu mkuu baada ya kupata upenyo alikimbia.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri hiyo, Juma Hamsini amesema tukio hilo ni utovu wa
nidhamu na ameandika barua Tume ya Utumishi wa Walimu kuchukua hatua haraka kwa
atakayebainika kuwa chanzo cha ugomvi huo.
Polisi
wilayani hapa wamesema wanaendelea na uchunguzi na wakikamilisha watatoa
taarifa ikiwemo kumfikisha mahakamani mhusika.
By
Antony Mayunga, Mwananchi
WALIMU WACHAPANA MAKONDE OFISINI HUKU WANAFUNZI WAKISHUHUDIA SERENGETI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment