Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM
Humphrey Polepole amesema CHADEMA wamefanya kikao cha dharura
kususia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata unaotarajiwa kufanyika January
13 mwakani.
Polepole amewatuhumu
CHADEMA kuwa wanatumia mgongo wa kuminywa kwa Demokrasia nchini kususia
uchaguzi huo wakati ukweli ni kwamba wamefulia baada ya kutumia vibaya hela ya
mfuko wa chama chao.
"Watani wanakutana leo, agenda
ni kutoshiriki uchaguzi unaokuja wa marudio kwa kisingizio cha demokrasia
lakini ukweli ni matumizi mabaya ya fedha yamefuja mfuko wa chama. Tafuteni
visingizio vingine lakini sio demokrasia. Watu wamechoka siasa za matukio.
Kikao chema!" Ameandika polepole katika ukurasa
wake wa Twitter.
olepole Awapiga Dongo CHADEMA.......Kadai Wamefulia, Wanajiandaa Kususia Uchaguzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment