Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda
Hindu alifariki dunia ghafla nyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Sakaya amesema Hindu alikuwa ni mpambanaji na mtu mwenye kukijenga chama hicho kuanzia miaka ya 90 hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.
‘’Hata ukifika Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.
“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.
No comments:
Post a Comment