MADEREVA 64 WA ARUSHA ,MANYARA,NA KILIMANJARO WAFUNGIWA LESENI KWA UZEMBE WA KUTOFUATA SHERIA ZA BARABARANI

Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani limewakamata madereva  64 wa mabasi ya abiria na kuwaweka rumande na kuzifungia kwa miezi 6 leseni zao katika mikoa ya arusha,manyara ,na Kilimanjaro waliokutwa na makosa mbalimbali ikiwemo kosa la mwendokasi katika oparesheni maalum ya jeshi hilo .

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchni Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Fortunatus Musilimu amesema oparesheni hiyo imetokana na mikoa ya kanda ya kaskazini kuwa miongoni mwa mikoa yenye ongezeko kubwa la ajali za barabarani hivyo wameamua kukomesha tabia hiyo na madereva wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani.

Bonyeza hapo chini umtazame kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini akizungumza kuhusu kufungia madereva hao.

MADEREVA 64 WA ARUSHA ,MANYARA,NA KILIMANJARO WAFUNGIWA LESENI KWA UZEMBE WA KUTOFUATA SHERIA ZA BARABARANI MADEREVA 64 WA ARUSHA ,MANYARA,NA KILIMANJARO WAFUNGIWA LESENI KWA UZEMBE WA KUTOFUATA SHERIA ZA BARABARANI Reviewed by KUSAGANEWS on September 10, 2017 Rating: 5

No comments: