IGP Sirro awashika koo wakina Simbachawene

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amewataka wale wote waliotajwa  katika ripoti ya biashara ya madini ya Almasi na Tanzanite wajasilimishe wao wenyewe katika ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kabla hawajakamatwa.

IGP Sirro ameelezaa hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema tayari wameshaanza kufanyia kazi ripoti waliyokabidhiwa na Rais Magufuli jana Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala ya  wizi, ufisadi, uzembe pamoja na rushwa zilizosababisha nchi kupata hasara kutokana na biashara ya madini.

"Wale wote waliotajwa kwenye ule uchunguzi wa biashara ya madini ni vizuri sana wakajisalimisha wao wenyewe kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili waweze kuhojiwa na uchunguzi ufanyike halafu tuweze kufahamu wanahusika kwa kiasi gani na wasisubiri kukamatwa. Kwa kuheshimu heshima zao ni vizuri wao wenyewe wakaja kuripoti kabla ya sheria kuchukua mkondo wake", amesema IGP Sirro.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika kamati ya uchunguzi wa biashara ya madini Almas na Tanzanite imeweza kuwataja  aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi pamoja na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

IGP Sirro awashika koo wakina Simbachawene IGP Sirro awashika koo wakina Simbachawene Reviewed by KUSAGANEWS on September 08, 2017 Rating: 5

No comments: