Jeshi la Polisi Tanzania limefanikiwa kushika nafasi tatu kwenye michezo ya majeshi ya polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO Games) iliyomalizika mjini Kampala, Uganda.Timu hiyo ya jeshi la polisi imefanikiwa kujinyakulia jumla ya medali sita ambapo moja ya dhahabu, mbili za fedha pamoja na medali tatu za shaba.
Wanamichezo hao wamepokelewa leo Makao Makuu ya Polisi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ambapo amesema Jeshi hilo litaendelea kushiriki michezo mbalimbali ili kuboresha mahusiano na kuiletea sifa nchi.
Kwa Upande wake mshindi wa medali ya dhahabu katika riadha mita 800 PC Basil John amesema michezo hiyo ilikuwa na ushindani mkubwa lakini walijitahidi kupambana ili kuhakikisha wanarejea na medali pamoja na uchache wao.
No comments:
Post a Comment