CUF yawakana wabunge wake

Chama cha Wananchi (CUF) upande unaomuunga mkono katibu mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, umetangaza kutowatambua wabunge wapya wa viti maalumu walioapishwa jana Septemba 5, bungeni mjini Dodoma.Akizungumza na wanahabari leo  jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Mbarawa Maharagande amesema wabunge hao wapya wamepatikana kwa njia isiyokuwa ya halali hivyo na kuwataka wanachama wasiwapatie ushirikiano.

"CUF  haina Wabunge wapya waliopitishwa na Vikao halali vya Chama na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa na kwa Spika kwa ajili ya Kuapishwa. Hao wanaoitwa ‘Wabunge walioapishwa’ wanaungwa mkono na serikali ya CCM hawatokani na chama chetu,"Maharagande.

Pamoja na hayo hayo Maharagande amesema kwamba kwa mara ya kwanza wabunge hao walioapishwa jana kupokelewa na kusindikizwa na wabunge wa CCM. 

"Wanaoitwa wabunge wa upinzani kuingia bungeni kuapishwa na kusindikizwa na wabunge wa CCM. CUF ikiwa Taasisi makini ya kisiasa nchini haitakubali kutumiwa kutengeneza upinzani feki wa kisiasa wa kuisaidia CCM iendelee kubaki madarakani. Tunatoa wito kwa wanachama na viongozi wote wa CUF nchini kutowapa ushirikiano wowote ule na kutowatambua kwa nafasi hizo za ubunge feki waliopewa na serikali ya CCM kwa lengo la kuihujumu taasisi ya CUF.

Maharagande ameongeza "Kila mmoja wetu mahala alipo achukue hatua za kudhibiti hujuma hizi za wasaliti wa Chama kwa kadri atakavyoweza" 

Pamoja na hayo Maharagande amesema "Huko nyuma tulikuwa na wabunge waliofukuzwa ndani ya chama na wanabakia kuwa wabunge wa mahakama na tulikuwa tukitumia terminology (istilahi) hiyo kwamba hawa ni wabunge wa mahakama lakini safari hii imekuwa tofauti".

CUF yawakana wabunge wake CUF yawakana wabunge wake Reviewed by KUSAGANEWS on September 06, 2017 Rating: 5

No comments: