Mbunge wa Nzega kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe amefunguka na kutaka katiba ya nchi kubadilika ili ikiwezekana kinga ya Rais iondolewe kwenye katiba kwa kuwa kinga hizi zinawafanya viongozi hao kufumbia macho baadhi ya vitu.Bashe amesema hayo leo mjini Dodoma baada ya kamati za bunge kutoa ripoti juu ya biashara za madini ya Tanzanite na Almasi ambapo katika ripoti hizo baadhi ya mawaziri wa serikali mbalimbali wametajwa kuhusika katika kufanya maamuzi ambayo yamelitia hasara taifa kwa maslahi yao binafsi.
"Umeona maamuzi yaliyofanywa na mawaziri waliotajwa kwenye hizo ripoti unatakiwa kujiuliza swali la msingi hivi maamuzi yote yale ya kuvunja sheria yaliyofanywa na mawaziri hivi Marais waliokuwa madarakani walikuwa hawajui? Leo Rais Magufuli asingekuwa tu amesukumwa na moyo wake kufanya haya anayofanya kwenye uwekezaji wa madini tungeyajua haya? Umefika wakati kama nchi wa kuangalia uwezekano kufanya mabadiliko ya katiba, tuangalie mabadiliko ya sheria tuangalie tunapowapa marais hawa kinga haya mambo ndiyo hutokea" alisema Bashe
Bashe anaamini kuwa maamuzi ambayo hufanywa na mawaziri hao ili kufanya mabadiliko makubwa katika baadhi ya mikataba ambayo imeigharimu serikali na nchi kiujumla kuwa ni lazima viongozi wao wa juu ambao ni Marais walikuwa wakitambua mambo hayo.
No comments:
Post a Comment