Wajawazito kusakwa mashuleni

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu amesema kamati ya ulinzi na usalama imekamilisha utaratibu wa kuwasaka wanafunzi wenye mimba ili kuchukua hatua inayostahili.Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo akiwa katika Kata ya Ntobo, kwenye  Halmashauri ya Msalala wakati wa makabidhiano ya mradi wa maendeleo ya jamii wa ADP Busangi uliotolewa na Shirika la World Vision Tanzania kwa ushirikiano na wananchi.

Nkurlu alisema pamoja na mafanikio ya mradi huo, kwa sasa tayari utaratibu wote kupitia kamati za ulinzi na usalama za mji, Msalala na Ushetu zimekaa na kukubaliana kufanya msako shuleni ili kuwabaini wasichana watakao kuwa na mimba.

“Baada ya kukubaliana kitakaochofuata ni kuwakamata na wale watakaobainika hatua kali zitachukuliwa, Serikali haiwezi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya watoto kwenda shule lakini yanafanyika mambo kinyume na malengo,”alisema.

Wajawazito kusakwa mashuleni Wajawazito kusakwa mashuleni


Reviewed by KUSAGANEWS on August 27, 2017 Rating: 5

No comments: