Akizungumza leo kwenye Planet Bongo
ya East Africa Radio, Roma amesema ingawa tayari idea ya wimbo huo
ilikuwepo lakini alitamani kuonyesha mama wa Afrika kwani Zimbabwe ni kati ya
nchi ambazo Tanzania ilisaidia kutafuta uhuru wake.
"Ningeweza kwenda Zimbabwe au
nchi nyingine yoyote Afrika lakini nilitaka kuonyesha Mama wa Afrika,
ukizingatia Rais Mandela na Nyerere tayari wameshaondoka lakini Mugabe yupo
hai. Nilipopata matatizo watu wa nchi mbalimbali walipaza sauti zao ili
tuliokuwa tumetekwa tupate kurudi tukiwa hai, kwa hiyo nikaona bora iwe
Zimbabwe ingawa tayari idea ya wimbo huu ilikuwepo muda mrefu kidogo" Roma.
Pamoja na hayo Roma amefunguka na
kusema wanaodhani kuwa Zimbabwe ni kubwa kuliko ngoma zake zote wanakosea kwani
wakati alipoingia kwenye game wimbo wake wa kwanza uliposikika redioni alipokea
simu nyingi za nje ya nchi kiasi cha kujihisi anaweza akaimba matatizo ya
wananchi wa Afrika na yakapatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo Roma ameweka wazi kuwa
bado anasafari ya Zimbabwe lakini hawezi kusema anakwenda kufanya nini
kwani ni mambo binafsi zaidi ingawa pia akimaliza 'media tour' ataondoka tena.
Roma atoa siri ya Zimbabwe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 21, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment