NA TUMAINI MAFIE ,ARUMERU.
KUTOKANA na uhaba wa vyumba vya madarasa wilayani Arumeru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekabidhi mabati 450 ili kutatua baadhi ya tatizo hilo kwa baadhi ya shule wilayani hapo.
Akikabidhi mabati hayo Leo kwa niaba ya Gambo kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya meru Happy Mrisho amesema yatasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua tatizo la uhaba wa madarasa katika Halmashauri hiyo ambapo aliwataka wanaufaika kutumia vyema mabati hayo ili kumaliza tatizo lililokuwa likiwakabili.
Aidha amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwapatia mabati hayo katika Halmashauri ya meru ambapo amesema yatasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa hususani sehemu husika kama alivyobaini katika ziara yake aliyoifanya siku chache zilizopita" alisema Bi Mrisho.
Amewataka waliopatiwa mabati hayo kukamilisha Ujenzi wa vyumba vya madarasa ili ifikapo Dec. Mwaka huu kazi hiyo iwe imeisha ambapo kata ya majengo wilayani hapo haikuwa na shule ya Sekondari , na mkuu wa mkoa aliahidi kutoa bati 100 ili kumalizia madarasa manne yaliyokuwa yameanzishwa ambapo inatarajiwa kuandikisha wanafunzi mwakani.
Wakitoa shukrani zao wakuu wa shule zilizopatiwa mabati hayo wamesema itawapunguzia mrundikano wa wanafunzi darasani ambapo walisema awali darasa moja lilikuwa likitumiwa na wanafunzi 60 jambo ambalo siyo sahihi Kwani idadi inayohitajika ni watoto 40 kwa kila darasa.
Kwa upande wa Mtendaji wa kata ya Legruki Abraham Pallangyo ambaye alikabidhiwa bati 100 amesema zitawasaidia kufanya ukarabati wa zahanati katika kata hiyo ambapo amesema zahanati iliyopo katika kata hiyo inaupungufu wa Wodi za kina mama wajawazito hivyo wanajenga wodi hizo kwa kutumia bati hizo ili kupunguza adha ya kina mama hao na wananchi wa kata hiyo kwa ujumla.
Hata hivyo mkuu wa mkoa akiwa ziarani wilayani hapo aliahidi kutoa bati 100,kata ya majengo kwa ajili ya kumalizia Ujenzi wa shule ya Sekondari ya kata hiyo, Bati 100, kata ya legruki ili kukarabati zahanati,ambapo kata nyingine alizoahidi ni pamoja na Maroroni na kata ya Malula inayoleta jumla ya bati 450.
No comments:
Post a Comment