Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la William Kimani Mwangi (32 )ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi nchini Kenya, baada ya kuibuka kwa ugomvi baina yao wakiwa bar.Mkurugenzi wa makosa ya jinai wa Limuru (DCIO) Mwenda Ithaiba, amesema siku ya Jumapili asubuhi alipokea taarifa za mauaji hayo yaliyotokea katika jimbo la Kiambu, ambapo walikuta mwili wa mtu huyo ukiwa kwenye gari yake.
Bwana Ithaiba aliendelea kusema kwamba polisi waliwahi eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu ukiwa kwenye kiti cha dereva na majeraha ya risasi kichwani mwake, huku injini ya gari ikiwa inaunguruma.
“Polisi inaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo, na mshukiwa ambaye pia ni askari polisi ameshamakatwa”, alisema DCIO Ithaiba
Kufuatia mashahidi wa tukio hilo wamesema marehemu alikuwa bar akipata kinywaji na marafiki zake, ndipo kukatokea mtafaruku baina yake na mtu mmoja ambaye alitambulika kuwa ni askari polisi, baada ya muda mfupi marehemu akaingia kwenye gari ili kuondoka, ndipo alipopigwa risasi wakati akijaribu kugeuza gari lake.
No comments:
Post a Comment