"NCHI YA TANZANIA SIYO MASKINI KATA BAADHI YA WATU WANAVYOSEMA "SIMBACHAWENE

Nchi ya Tanzania kwa mwaka 2016 imejitosheleza kwa upande wa upatikanaji wa chakula kwa asilimia 123 huku mwaka 2017 Ikijitosheleza kwa asilimia 120 licha ya kuwepo kipindi cha ukame hivyo Tanzania si maskini kama baadhi ya watu wanavyosema.

Hayo yamesemwa na waziri wa TAMISEMI George Simbachawene wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 24 ya wakulima na wafugaji kikanda yanayofanyika mkoani Arusha kwenye viwanja vya nane nane Themi Njiro.

Simbachawene amesema kuwa katika sekta ya kilimo kuna udalali ambao siyo mzuri ambao unaweza kuidimiza sekta ya kilimo na kufanya sekta hiyo kuonekana kuwa ni mbovu kwa wakulima hivyo atangalia jinsi ya kusemea jambo hilo licha ya kuwa halihusiki na ofisi yake.

Pamoja na hayoamewataka wakuu wa mikoa kusimamia vema maeneo yao kwasababu wao ndiyo kila kitu katikamaeneo yao ili kufikia malengo ambayo watanzania wameyalenga ili kuwatoa kwenye umaskini 

Kwa upande wa mkuu wa mkoa Wa Arusha Mrisho gambo amesema kuwa kamati aliyoiunda kuchunguza mali zilizpo katika uwanja huo wa TASO njiro inaendelea na wataipokea katika makabidhiano ya uwanja huo na itahusisha mikoa yote mitatu.

Naye meya wa jiji la Arusha Mh KALIST lazaro amesema kuwa malengo ya serikali kuchukua maonyesho hayo kutoka kwa taso ni jambo jema kwasababu kila kitu kitakuwa wazi.
"NCHI YA TANZANIA SIYO MASKINI KATA BAADHI YA WATU WANAVYOSEMA "SIMBACHAWENE "NCHI YA TANZANIA SIYO MASKINI KATA BAADHI YA WATU WANAVYOSEMA "SIMBACHAWENE Reviewed by KUSAGANEWS on August 05, 2017 Rating: 5

No comments: