Na Hababi Mohammed
Wanaharakati wa masuala ya kijamii,siasa kutoka nchi kumi za afrika wamekutana jijini arusha kwa ajili ya kuadhimisha azimio la kilimanjaro lengo kuu la maadhimisho hayo ni kimuhamasisha mwafrika katika kupigania Haki,amani back heshima katika nchi zao.
Omboki otieno ni mwanaharakati kutoka nchini Kenya ambae amelezea malengo ya harakati hizo huku akisisitiza suala kupiga vita umaskini kwa nchi za afrika na kutoa rai kwa wananchi kuwa na tamaduni ya kuto tegemea wanasiasa kwa ajili ya kuleta maendeleo katika nchi na utunzaji wa Mali asili.
Katika hatua nyingine otieno amesema nchi nyingi za afrika kumekuwa na kasumba ya matumizi hasi ya rasilimali na kuto nufaisha walengwa katika eneo husika na kutoa fursa sawa kwa wazawa suala ambalo bado huchangia kumdidimiza mwanamke na kijana katika kuleta fursa chanya za kimaendeleo.
Imeelezwa kuwa nchi nyingi za bara la afrika Suala la democrasia bado limekuwa ni changamoto kwa maslahi ya wananchi wa mataifa hayo Kama anavyo Elezea mmoja wa washiriki kutoka D R C Congo.
Miongoni mwa nchi zinazo shiriki Katika maadhimisho hayo pamoja na kujifunza mambo mbalimbali kwa ajili kutetea haki,amani na utu wa mwafrika,ni nchi ya Senegal, Kenya, Morocco Congo, Liberia, Somalia, Burundi, Uganda Benin,na wenyeji Tanzania.
Mwisho
No comments:
Post a Comment