NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA
WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita amesema kuwa ipo haja ya kuangalia nijinsi gani watu wenye
kipato duni na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaweza kufikiwa na
kuelimishwa umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya.
Meya Mwita amesema hayo jijini hapa
leo wakati alipokuwa akifungua mkutano wasiku mbili wa wadau wa kujadili
upatikanaji wa huduma za afya kwa makundi maalumu sambamba na ukiwa na lengo la
kuboresha upatikanaji wa huduma hizo kwa watu wenye kipato cha chini.
Amefafanua kuwa watu wenye kipato
cha chini ,makundi mbalimbali wanashindwa kuwa na huduma hiyo kutokana na
kukosa uhamasishaji, elimu ya kutosha hivyo akashauri kuwa ni vyema jambo hilo
likazingatiwa kwenye maeneo yote.
“ Tunapozungumzia huduma bora za afya
kwa wakazi wa jiji letu, tuliangalie pia eneo la gharama za utoaji
wa huduma, namna tunavyoweza kuihamasisha jamii kujiunga na bima ya afya
ili kumsaidia na kumhakikishia mwananchi kupata huduma hiyo pale
anapozihitaji” amesema Meya Mwita.
Ameongeza kuwa kwakuwa jiji la Dar
es Salaam linaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu ni muhimu kuhakikisha nguvu
kazi iliyopo jijini hapa ni ile watu wake wana afya njema.
Amesema jambo la msingi katika
majadiliano ya mkutano huo, ni kuainisha hatua zinazo hitajika kuchukuliwa ili
kuhakikisha wakazi wa jijini hapa ,hususani wale wenye kipato cha chini na
waishio kwenye mazingira magumu wanafikiwa na kupata huduma bora za afya.
Hata hivyo alisema kulingana na
takwimu za sense ya Taifa ya mwaka 2012, jiji la Dar es Salaam linakadiriwa
kuwa na takribani watu milioni 4.4 hivyo kwa kuzingatia hilo ni muhimu kuwa na
mipango madhubuti ambayo itawawezesha wakazi wake kupata huduma bora za
kijamii, hususani za kiafya.
Jiji la Dar es Salaam limekuwa na
ushirikiano na urafiki wa jiji la Hamburg kwa kipindi cha miaka 10, mkutano huo
ni mwendelezo wa juhudi za wadau na Taasisi ndani ya majiji haya katika
kuendeleza utamaduni wa undugu na urafiki uliopo.
Mkutano huo umehusisha , Tume ya
Kikristu ya huduma za jamii (CSSC), marafiki kutoka Diakonie ya Hamburg
Ujerumani, Madiwani kutoka kata za Mtoni Mtongani, Ukonga, Buguruni na
zinginezo.
Meya Mwita ashauri Wananchi wenye kipato duni, mazingira magumu wapatiwe elimu kuhusu Bima ya Afya.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment