Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Mh.
God Bless Lema amelaani vikali kitendo cha Mbunge mwenzake Ester Bulaya wa
Bunda kukamatwa na kuwekwa Rumande kwa amri ya Mkuu wa Wilaya kwa madai kuwa
hakuna sheria Tanzania inayokubali vitendo hivyo.
Akizungumza
ofisini kwake mapema leo asubuhi, Lema amesisitiza kuwa vitendo hivyo ni
muendelezo wa uvunjifu wa amani huku akihofia kwamba nchi inapoelekea ni
kubaya hasa mbegu za chuki ambazo zinapandikizwa zinaweza kuleta mpasuko mbaya
katika taifa.
Mh.
Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa mambo ya ndani amesema kuwa kosa
lililomuweka ndani Mh. Bulaya la kushiriki mkutano wa hadhara uliofanyika
Tarime halipo katika sheria ya Tanzania na hata ikifanyiwa marekebisho hakuna
sheria inayomzuia mtu kuzungumza katika mipaka ya taifa lake.
"Kama mbunge niliyepitia madhila mengi
yakiwepo ya kukamatwa na polisi mara kwa mara hili jambo
linasikitisha sana kwamba Mbunge amekamatwa kwa sababu ya kwenda kuhudhuria au
kuhutubia jimbo lingine, Wakati Mbunge anaruhusiwa kuhutubia mahali popote
ndani ya mipaka ya Tanzania ndiyo maana anaitwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, hata wewe Mwandishi au mtu wa kawaida. Hii ni hatari kwa
nchi"
Tunapoelekea wasukuma watasema
hawawataki wachaga usukumani yaani tutaanza kukataana. Hii mbegu siyo kwamba tu
inauua demokrasia, uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kutembea popote kama katiba
inavyoainisha lakini kinatengeneza mpasuko mkubwa katika taifa. Mbegu hii ikiota
italeta machafuko makubwa hapo mbeleni.
Lema
ameongeza kuwa tabia zinazofanywa na viongozi wa serikali zinawapa nafasi
wananchi kutenga watu kwa kabila zao, ukanda wao.
"Kitakuja kizazi ambacho hakitataka
kuzungumza kupitia vipaza sauti au mitandao ya kijamii au kwenda kulilia kwenye
mataifa mengine na badala yake vitafuata usemi wa jino kwa jino. Nazungumza
hivi kwa sababu naipenda nchi yangu" Lema
Lema awaka kukamatwa kwa Bulaya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment