Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekemea matukio ya utekaji watoto yaliyoibuka katika siku za karibuni jijini Arusha na ameitaka Serikali ichukue hatua.
Lema ametoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkeryan, Daud Safari.
Amesema hadi sasa watoto wanne wanadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana hali ambayo imeibua hofu na shaka kwa wakazi wa Jiji la Arusha.
Lema amesema watoto wadogo wamekuwa wakitekwa katika mazingira tofauti na watekaji kudai kiasi kikubwa cha fedha.
Mbunge huyo ametaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuingilia kati matukio hayo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkeryan, Safari amesema hadi sasa watoto wanne ndani ya wiki moja wametekwa na hawajulikani walipo.
No comments:
Post a Comment