Ikiwa ni siku moja imepita tangu Bunge jamii ,kuwa na mjadala wa kina kuhusu vijana wanaopoteza muda mitandaoni kujadili maswala yasiyo na faida huku wengi wakikaa bila kazi.
Naibu waziri wa naibu waziri sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye ulemavu,Anthony Mavunde ameunga mkono kauli hiyo wakatu wa uzinduzi wa mafunzo ya utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi kwa vijana 847 kutoka mikoa ya mtwara,Lindi,Morogoro,Pwani,na Daresalam.
Akizungumza Mavunde amewataka Vijana kuchangamkia fursa wasisubiri serikali itoe matangazo ya ajira kwa kuwa kila maisha ya kijana wa Kitanzania yananzia nayeye mwenyewe kwa kwa kujiamini ili kutimiza malengo.
Ameongeza kuwa,kila kijana aliyepata fursa ya kuingia kwenye Mafunzo Hayo, watimie vizuri fursa hiyo kwa kujiwekea uaminifu na uwajibikaji kama msingi wa mafanikio, na kuacha Tamaa ili waende kwa Hatua.
"ni kaburi peke yake watu waanza kuchimba kuanzia juu kwenda Chini, lakini maisha yananzia Chini kwenda juu" amesisitiza Mh Mavunde.
Mafunzo hayo yametolewa na Serikali kupitia Fedha za walipa Kodi, hivyo Mavunde amewaomba vijana wahakikishe wanatumia vizuri fedha zinazotolewa katika mafunzo Hayo maana ni fedha za watanzania,ambapo Serikali ya Mhe John Pombe Magufuli imedhamiria kuwekeza kwa vijana kwa kuwajengea uwezo vijana ili waweze kunufaika na maendeleo ya rasilimali zilizopo nchini
Malengo ya serikali ni kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati na yenye viwanda
po
No comments:
Post a Comment