WAZIRI DKT. MPANGO AHIMIZA UCHUMI WA VIWANDA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adam Msumule akitoa elimu ya Bajeti kwa wananchi waliotembelea katika banda la Wizara hiyo katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana mkono na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, walipokutana katika viwanja vya Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhusu namna ya kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kukata bima ili kujikinga na majanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lilipo katika viwanja vya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Sam Kamanga.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Naftal Sigwejo baada ya kuulizwa kuhusu ubora wa baadhi ya bidhaa zinazotolewa Serikalini baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka Mfuko wa Pensheni wa GEPF kuhusu huduma na mchango wa mfuko huo katika maendeleo ya viwanda, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipata maelezo kutoka  Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu njia ya kisasa ya ufugaji Samaki alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akimpongeza mtumishi wa Suma JKT baada ya kutoa maelezo ya mtambo wa kuvuta maji katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

WAZIRI DKT. MPANGO AHIMIZA UCHUMI WA VIWANDA KATIKA MAONESHO YA SABASABA WAZIRI DKT. MPANGO AHIMIZA UCHUMI WA VIWANDA KATIKA MAONESHO YA SABASABA Reviewed by KUSAGANEWS on July 09, 2017 Rating: 5

No comments: