Mkapa awasili Chato kukabidhi Nyumba 50 za watumishi wa afya

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amewasili wilayani Chato kwa ajili ya kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa afya wilayani humo.

Makabidhiano hayo yanafanyika leo (Jumapili, Julai 10) kwa niaba ya mikoa mingine mitatu ambayo pia imejengewa nyumba hizo n Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Taarifa iliyotolewa  jana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa tasisi hiyo, Richard Bagolele, imeeleza kuwa Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida ataungana na Rais Mkapa kukabidhi mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti. Mtambo huo umejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

Kesho, Rais John Magufuli ambaye yupo mapumziko wilayani Chato, atashiriki katika hafla ya makabidhiano hayo yatakayofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu Chato.

 



Mkapa awasili Chato kukabidhi Nyumba 50 za watumishi wa afya Mkapa awasili Chato kukabidhi Nyumba 50 za watumishi wa afya Reviewed by KUSAGANEWS on July 09, 2017 Rating: 5

No comments: