Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mauaji ya jeshi la Polisi na wananchi kiujumla hayawezi kuvumilika kuona yanaendelea kutokea huku akituma ujumbe mzito kuwa wanaweza kukimbia na kujificha wauaji lakini watakamatwa tu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa amebainisha hayo leo bungeni wakati akihitimisha mkutano wa saba wa bunge uliofanyika jijini Dodoma baada ya kuendelea vitendo vya viovu vya kihalifu vinavyotokea huko Mkoani Pwani hasa wilaya ya Kibiti na Rufiji.
"Mauaji ya wananchi wetu na jeshi la polisi hayakubariki na wala hayavumiliki kwani askari ni walinzi wetu, serikali imelaani kitendo hicho na itahakikisha waliofanya vitendo hivyo watakamatwa", amesema Majaliwa.
Mbali na hilo, Waziri Mkuu amesema serikali ya awamu ya tano imetenga takribani shilingi bilioni 7 kwa ajili ya kusaidia kununua vifaa tiba pamoja na dawa zitakazoweza kuwasaidia kunusuru uhai wa mama na mtoto wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment