JPM, Mkapa wawasili Uwanja wa Mzaina chato

       Rais John Magufuli na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wamewasili katika uwanja wa mpira wa miguu wa Mzaina, Chato leo Julai 10.

Rais Magufuli anatarajiwa kuhutubia katika hafla ambayo pia Balozi wa Tanzania Japan, Masaharu Yoshida atakabidhi mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti.

Mtambo huo umejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

Jana, Rais Mkapa alizindua nyumba 50 za wahudumu wa afya zilizotolewa kwa hisani ya Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.

Kwa sasa viongozi mbalimbali wa dini wanafungua hafla hiyo kwa sala. 


JPM, Mkapa wawasili Uwanja wa Mzaina chato JPM, Mkapa wawasili Uwanja wa Mzaina chato Reviewed by KUSAGANEWS on July 10, 2017 Rating: 5

No comments: