Mwili wa
marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao Igokero
wilayani Misungwi.
Shughuli
ya kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo
ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha
Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulusubisya.
Akizungumza
katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia kwa kipindi
alichokuwa amelazwa hospitalini hapo.
“Nawapongeza
Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini
kazi ya Mungu haina makosa , pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi
wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye hivyo hata kwa wazee
wengine’’ amesema Katemba.
Naye Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga amesema walimpokea
Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokua akipatiwa
matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua kwamba ana maradhI ya
Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua
akiishi.
Hivyo Dk.
Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini mapema pindi
mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi hospitali ni rahisi
kupata tiba na kupona kuliko kusubiri hadi ugonjwa uwe sugu.
Mzee
Francis Maige Kanyasu alizaliwa 1931 na kufariki dunia Mei 29 , 2017 saa mbili
na nusu usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu ‘Ngosha’ Wasafirishwa Mwanza leo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment