HALMASHAURI ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa
Pwani itaanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kuhusu kuhakiki
mipaka inayotenganisha vijiji na Hifadhi ya Saadani mara baada ya mvua
kumalizika.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Said Zikatimu katika Baraza la Madiwani akitolea ufafanuzi iliyokuwa
inazungumzia migogoro ya mpaka kati ya wananchi wa vijiji husika na Hifadhi
ambapo alisema mara baada ya mvua hizo kwisha kazi hiyo itaanza mara moja.
Baraza hilo likihudhuliwa na Mhifadhi Mwandamizi wa
SANAPA Lumi Ole Naikasi, madiwani hao walitaka kufahamu kutoka kwa Mhifadhi
huyo kwamba ni lini mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi na wananchi hao
utamalizika, wengine wakiulizia hatima ya malipo kwa wananchi ambao wametoa
maeneo yao kwa hifadhi hiyo.
Rehema Mno alizungumzia suala linalohusiana na tozo
ya sh. 5,000 kwa wananchi wanaokwenda kwenye vijiji hivyo kuangalia familia zao
ambao wanapofika katika mlango wa kuingia ndani ya hifadhi wanatizwa fedha
jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi hao.
Sijali Mpwimbwi alitaka kujua hatma ya migogoro ya
mipaka kati ya wananchi na Hifadhi pia malipo ya fidia kwa waliotakiwa kuondoka
kwenye maeneo yao, huku Hussein Hading'oka akisema ingawa Hifadhi imewekwa kwa
makusudi maalumu kwa mujibu wa sheria na Taratibu, huku ikiwakuta wananchi,
sasa imekuwa kero kwao.
"Saadani haina tofauti na Hifadhi nyingine,
nichukulie mfano ya Mikumi ina urefu wa zaidi ya kilomita 50 kutoka kona mpaka
kona lakini watu wanapita muda wote hakuna kuzuiwa, iweje Saadani wananchi wetu
wazuiwe baada ya saa 12 za jioni?," alihoji Hading'oka.
Juma Mpwimbwi alisema kuwa Halmashauri inamiliki
kilometa 45 za barabara wakati TANAPA ina kilometa si zaidi ya 12, lakini
wanatoza uahuru kwa kila gari zaidi ya sh. Laki moja, barabara zinapoharibika
hawafanyi mateengenezo hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria
wanaosafiri kwa magari, huku akigusia kuzuiliwa kwa gari la kubeba wagonjwa
kuoita enwo hilo.
"Cha kusikitisha zaidi hata panapotokea mgonjwa
wakipiga simu kwangu ili gari ya wagonjwa iende, ikifika mlangoni wanaizuia
wakieleza muda wa kupita eneo hilo unekwisha, wale ndugu zetu wataishije?
Alihoji Mpwimbwi.
Akizungumzia malalamiko hayo, Mhifadhi Lumi alisema
kuwa suala la ushuru wa kuingia ndani ya eneo la Hifadhi upo kisheria hivyo wao
hawawezi kutengua, kuhuau mipaka wao wameikuta, wakati upande wa fidia kwa
wananchi kufuatia maeneo yao kuchukuliwa, wapo tayari kuwalipa wanachosubiri ni
taratibu.
Akihitimisha mjadala huo, Zikatimu alisema kwamba
kuhusu mipaka kuna maelekezo yametolewa na Waziri Mkuu Majaliwa na kwamba mara
baada ya mvua za masika kaI hiyo itafanyika.
Chalinze Kutekeleza Agizo La Majaliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment