Kufuatia kifo cha mmoja wa Waasisi wa
CHADEMA, Mzee Philemon Ndesamburo Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo, (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji, ametoa maelekezo kwa watendaji
nchi nzima kupeperusha bendera nusu mlingoti.
Amesema Chama kitashiriki katika msiba huo kwa heshima zote ili kumuenzi mmoja wa waasisi wa siasa za mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli nchini.
Amesema kuwa msiba huo ni msiba wa CHADEMA, ni msiba wa Watanzania, ni msiba wa Taifa lote kutokana na mchango mkubwa wa Mzee ndesamburo kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa nchi ya Tanazania na ndiye aliyekifadhili Chama kwa mara ya kwanza kwa kukipatia ofisi eneo la Kisutu jijini Dar es salaam.
CHADEMA kupeperusha bendera nusu mlingoti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 01, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment