****Mtu mmoja amejinyonga hadi kufa
kwa kutumia kamba ya katani wilayani nyamagana.
****Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi
la polisi kwa kosa la kupatikana akiwa na pombe iliyohifadhiwa kwenye
vifungashio vya plastiki almaarufu viroba pakiti 103 wilayani ilemela.
Kwamba tarehe 23.04.2017 majira ya
18:45hrs jioni katika mtaa wa mkuyuni sokoni kata ya mkuyuni wilaya ya nyamagana
jiji na mkoa wa mwanza, mtu mmoja mwanamume aliyrfahamika kwa jina la faraja
anselem miaka 31, mkazi wa mtaa wa mkuyuni sokoni, alikutwa akiwa amejinyonga
chumbani kwake hadi kufariki dunia kwa kutumia kamba ya katani aliyokua
ameifunga kwenye paa la chumba, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Inasemekana kuwa taraehe tajwa hapo
juu marehemu alibaki mwenyewe nyumbani, aidha inadaiwa kuwa kabla ya kufanya
tukio hilo marehemu alionekana akiingia chumbani kwake kisha akafunga mlango
ndipo baada ya muda kupita watoto waliokua wakicheza maeneo hayo waliona miguu
ikining’inia dirishani ndipo walitoa taarifa kwa wazazi wao.
Majirani baada ya kuona tukio hilo
walitoa taarifa polisi, ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo
la tukio na kuukuta mwili wa marehemu ukining’inia mahali hapo, mwili wa
marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi
pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya
mazishi. Aidha upelezi kuhusiana na kifo hicho bado unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza
naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa
wa mwanza, akiwaomba kuwa pale watakapoona mtu amekuwa na msongo wa mawazo kwa
muda mrefu hadi inapelekea kuweza kufanya kitu kisicho cha kawaida cha kuweza
kujidhuru yeye mwenyewe au watu wengine, wamfikishe kwa wataalamu wa ushauri
nasaha ili waweze kumshauri na kumwaondoa katika hali hiyo ya msongo wa mawazo
na kisha kurudi katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na maisha.
Katika tukio la pili,
Kwamba tarehe 23.04.2017 majira ya
saa 14:33hrs katika mtaa wa kiloleli kata ya nyamanoro wilaya ya ilemela jiji
na mkoa wa mwanza, askari wakiwa doria na misako walifanikiwa kumkamata mtu
aliyefahamika kwa jina la donatus sebastina miaka 16, mkazi wa kiloleli akiwa
na pombe iliyeowekwa kwenye vifunganishio vya plastiki almaarufu viroba aina ya
empire pakiti 103, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Awali askari wakiwa kwenye doria na
misako walipokea taarifa kutoka kwa wasiri kwamba maeneo tajwa hapo juu yupo
mtu anayefanya biashara ya kuuza pombe ya viroba kwa siri, kutokana na taarifa
hizo askari walifanya upelelezi wa kimyakimya huku wakiendelea na doria ndipo
baada ya muda waliweza kufahamu mahali anapoishi mtuhumiwa na kufanikiwa
kumkamata akaiwa na pakiti 103 za pombe iliyohifadhiwa kwenye vifungashio vya
plastiki almaarufu viroba aina ya empire.
Mtuhumiwa yupo katika mahojiano na
polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakani, aidha upeleezi na
misako ya kuwatafuta watu wengine wanaojihusisha na biashara hiyo ya pombe za
viroba bado unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza
naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa
wa mwanza akiwataka kuendelea kutoa taarifa mapema kwa jeshi la polisi ili watu
wanaojihusisha na biashari hiyo ya pombe za viroba waweze kukamatwa na
kifikishwa katika vyombo vya sheria.
Imetolewa na:
Dcp: Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza
Mtu mmoja Amejinyonga hadi kufa kwa Kutumia Kamba ya Katani Mkoani Mwanza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment