Meya wa Jiji Arusha atembelea machimbo ya makaa ya Mawe ya UNESCO -WELTERBE ZOLLVEREIN



Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro,ameendelea na ziara ughaibuni ambapo jana alisafiri na treni ya mwendo kasi(fast train) kutoka Brussels-Belgium kwenda Mji wa Essen Germany ambapo alipokelewa na Lord Mayor wa Essen City Honorable Thomas Kufen nakufanya naye mazungumzo ya kina juu ya mahusiano ya Miiji hii miwili/Sister ship (Essen City – Germany & Arusha City-Tanzania) 

Essen City Lord Mayor Hon Thomas Kufen alipewa tuzo ya "The Green Capital City in Europe" na European Union mwaka 2017. 

Mji huu ni Mji wa Viwanda hasa Coal Mining and Steel hivyo kuwa moja kati ya Miji michafu mwaka 1923 hadi 1993.Kwa jitihada zilizofanyika sasa ndio The Green City in Europe. 

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro pia alifanya mazungumzo na Municipal Director on Climate Agency wa Mji wa Essen,pia alifanya mazungumzo na Simone Raskop Head of Department in Manicipalities on Planning and Reneable Energy, 

Jioni Mstahiki Meya wa Jiji Arusha alitembelea machimbo ya makaa ya Mawe -caol mining na makumbusho ya COAL MINING ambayo sasa yanaitwa UNESCO -WELTERBE ZOLLVEREIN (Former mine turned into an UNESCO heritage industrial and architectural monument). Ambapo kwa sasa Germany karibu imeyafungia machimbo yote ya makaa ya mawe kasoro machimbo mawili ambapo yanayotarajiwa kufungwa mwaka 2018 kwani kwao ni gharama kubwa kuchimba na kwa sasa wanaagiza kutoka nchi za Colombia,Latin America na Belgium ambapo ni rahisi kwa sasa. 

Chanzo msumba news
Meya wa Jiji Arusha atembelea machimbo ya makaa ya Mawe ya UNESCO -WELTERBE ZOLLVEREIN Meya wa Jiji Arusha atembelea machimbo ya makaa ya Mawe ya UNESCO -WELTERBE ZOLLVEREIN Reviewed by KUSAGANEWS on April 28, 2017 Rating: 5

No comments: