Mbunge wa Nzega mjini, Hussein Mohamed
Bashe amesikitishwa na Serikali ya Kenya kuweka zuio la kuingiza mitungi ya
gesi inayotoka Tanzania kwa kusema ni vizuri nchi hiyo ikaheshimu mikataba ya
'East African Community (EAC)' .
Bashe amesema hayo baada ya serikali
ya Kenya kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Andrew Kamau
kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya kupikia kutoka Tanzania kupitia mipaka ya
nchi hiyo.
"Serikali ya Kenya imezuia gesi
za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tanzania kuingia Kenya ni vizuri Kenya
ikaheshimu 'EAC treaty common'......Dar es salaam 'port and Cost' ya gesi
inayotoka Tanzania ndiyo 'competetive edge' ya makampuni ya Tanzania dhidi ya
yale ya Kenya uamuzi huu si sawa". Ameandika
Bashe kupitia ukurasa wake wa twitter.
Hussein Bashe Aipa Makavu Serikali ya Kenya Kwa Kuzuia Gesi ya Tanzania
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment