Hofu huzuni na majonzi vimetanda kwa madereva ambao ni wanachama wa chama cha madereva nchini waliokuwa wamekusanyika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kupata taarifa kuwa katibu na msemaji wa chama cha madereva nchini Bwana Rashid Salehe amefariki dunia baada ya kugua gafla ugonjwa usiojulikana.
katika hospilati ya Muhimbili ilikuwa madereva wameketi mafungumafungu huku wakiwa wamejawana majonzi mazito na kudai kutoamini kilekilichotokea baada ya kupata taarifa kuwa katibu na msemaji wao amefariki dunia katika mazingira ya kifo chake ambacho wamedai kimegubikwa na utata mkubwa na kuomba madaktari kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha kifo chake kama anavyobainisha mwenyekiti wa chama cha maderva nchini Bwana Shaban Mdemu.
Muda mfupi baadae mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadiki naye aliunga na madereva hao na kuelezea kushitushwa na kusikitishwa na kifo cha Rashid Salehe na kusema amefariki kipindi ambacho mchango wake muhimu ulikuwa unahitajika katika kutanzua matatizo yayowakabili madereva nchini na kulazimika kuagiza jopo la madaktari wa Muhimbili kufanya uchunguzi wa kina kwa mwili wa katibu huyo wa madereva ili kujua chanzo na sababu ya kifo chake.
Wiki moja kabla kugua gafla na kufariki kwa katibu na msemaji wa chama cha madereva nchini Bwana Rashid Salehe alisema changamoto zinazowakabilia madereva hasa katika mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC nani hatua gani chama chake kinachukau.
Katibu na msemaji wa chama cha madereva nchini Rashid Salehe afariki dunia gafla.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 22, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment