Wafanyikazi 20 wa uma nchini Tanzania walifungiwa kwa hadi saa sita kwa kuchelewa kazini.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni mjini Dar es Salaam aliagiza kukamatwa kwao
baada ya maafisa hao kuwasili kazini wakiwa wamechelewa kwa saa tatu.Mkutano huo kati ya mkuu huyo wa Wilaya Paul Makonda na maafisa hao 20 ulilenga kusuluhisha mgogoro mrefu wa ardhi katika eneo hilo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa alilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuwangojea maafisa hao kwa saa tatu.
Na walipowasili walikuwa hawana sababu ya kuchelewa kwao.
Ni wakati huo ambapo bwana Makonda aliwaagiza maafisa wa polisi kuwakamata na kuwafungia.
Kuchelewa na mapumziko ya chai ya saa nne ni miongoni mwa malalamishi yanayotolewa na raia wanaotafuta huduma katika afisi za uma.
Habari kuhusu vitendo vya mkuu huyo wa Wilaya zimekuwa zikisambaa katika vyombo vya habari huku raia wengi wa Tanzania wakiunga mkono hatua yake.
Hatahivyo mashirika ya haki za kibinaadamu yamekosoa hatua hiyo yakisema kuna sheria zinazofaa kufuatwa ili kuzuia ghasia.
Maafisa hao baadaye waliwachiliwa huru huku mkutano huo ukifanyika asubuhi ya Alhamisi baada ya maafisa hao kuwasili saa mbili kabla ya mkutano huo.
Hatua hiyo inaonekana kama harakati ya kuweka maadili ya kufanya kazi miongoni mwa wafanyikazi wa uma kama inavyotakiwa na rais John Pombe Magufuli.
BBC
DC awafungia maafisa waliochelewa kazini TZ
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 26, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment