Watanzania wametakiwa kuwapuuza wanasiasa wanaotumia vyombo vya habari kwa manufaa yao binafsi ya kisiasa hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.
Rai hiyo kwa watanzania imetolewa jijini Dar es salaam na
mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere Bw Joseph Butiku
ambapo amesema nivema wanasiasa na seriakli kwa ujumla wakaacha
kuwatisha watanzania kwa kutumia vyombo vya habari.
Akitoa mada katika mdahalo ulioandaliwa na taasisi hiyo ya Mwalimu
Nyerere, Prof Mwesiga Baregu amesema ni vema katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mkuu vyama vya siasa vikawa mstali wa mbele katika
kuhakikisha taifa linavuka salama.
Bw Hamphrey Polepole alikuwa ni miongoni mwa watoa mada wakuu aktika mdahalo huo ambapo suala la katiba lilizungumza.
Watanzania wametakiwa kuwapuuza wanasiasa wanaotumia vyombo vya habari kwa manufaa yao binafsi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment