RUTO ataka ushirikiano kukabiliana na ugaidi

Naibu Rais wa KENYA, WILLIAM RUTO amewataka wadau wa masuala ya usalama kutoka nchi 40, wanaohudhuria mkutano wa usalama nchini humo kushirikiana kuzindua mikakati mipya kukabiliana na vitendo vya ugaidi duniani. 

Wajumbe wapatao 300 wanaohudhuria mkutano huo nchini KENYA wanajadiliana pia jinsi ya kukabiliana na mafunzo yenye itikadi kali, yanayowavutia vijana wengi kujiunga na makundi ya kigaidi kama vile AL-SHABAB. 

RUTO ameonya kuwa dhamira ya vikundi mbalimbali vya kigaidi kama AL SHABAAB kuanzisha taifa jipya la kiislamu katika Pembe ya AFRIKA halitafanikiwa. 

Amesema kikundi hicho kimekuwa kikitoa mafunzo kwa vijana wanaokuwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na magerezani ili hatimaye wawe magaidi wa kimataifa na kwenda kuhatarisha usalama katika nchi zingine. 

Mkutano huo wa wadau wa usalama unafanyika wakati kuna habari kuwa limetokea shambulio lingine la kigaidi huko LAMU nchini KENYA.
RUTO ataka ushirikiano kukabiliana na ugaidi RUTO ataka ushirikiano kukabiliana na ugaidi Reviewed by KUSAGANEWS on June 26, 2015 Rating: 5

No comments: