Wadau wa elimu mkoani Ruvuma wamesikitikitishwa na kiwango
kikubwa cha wanafunzi kumaliza elimu ya msingi wakiwa hawajui kusoma na
kuandika hali inayosababisha kuzalisha wasomi walio na uwezo mdogo hivyo
wametoa mapendkezo ya kukomesha hali hiyo.
Wakizungumza katika Maadhimisho ya wiki ya Elimu mkoani
Ruvuma wamesema kuwa kunatakiwa mabadiliko makubwa ya mitihani ili kuweza
kuzalisha wanafunzi wenye uwezo kuliko mitihani ya sasa ya kuchagua ambayo
inamfanya mwanafunzi kufaulu elimu ya msingi akiwa hajui kusoma na kuandika.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Ephraim
Simbeye anasema kuwa mkoa wa Ruvuma unafafanya jitihada kupunguza idadi kubwa
ya wanafunzi wasioujua kusoma, kuandika na kuhesabu
Naye Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme anatoa
maagizo kwa walimu na maofisa elimu kuondoa tatizo la wanafunzi kumaliza elimu
ya msigi wakiwa hawajui kusoma, kuhesabu na kuandika .
Wanafunzi waliomaliza Elimu ya Msingi Ruvuma hawajui Kusoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment