Vurugu zaibuka Kwenye Marudio ya uchaguzi Mdogo Jijini Arusha, Polisi wachunguza

Jeshi la polisi mkoani Arusha limefungua jalada la uchunguzi wa matukio ya vurugu katika uchaguzi kata ya Kaloleni jijini Arusha baada ya watu wawili kuchomwa visu huku mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema akishushiwa kipigo

Akizungumza  leo Jumapili Agosti 12, 2018 kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi amesema Lema ametoa taarifa za kushambuliwa sambamba na mgombea wa chama hicho katika kata hiyo, Boniface Kimario pamoja na wakala wake

Amesema baada ya taarifa hiyo, majeruhi walipelekwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru wanakoendelea na matibabu

“Tumefungua jalada la uchunguzi na tunawasaka waliohusika,” amesema

Katika tukio hilo, Lema anadaiwa kushushiwa kipigo na watu wanaodaiwa kuwa walinzi wa CCM wakimtuhumu kutaka kufanya vurugu eneo la Tangi la Maji

Mbali na Lema, wakala wa Chadema, Ibrahim Ismail amechomwa visu na kulazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru

Katika vurugu hizo, pia inadaiwa mwenyekiti wa CCM kata ya Kaloleni, Iddi Mukuru amejeruhiwa kwa kuchomwa visu

Akizungumza mgombea wa CCM katika kata hiyo, Emmanuel Kessy amesema licha ya vurugu hizo uchaguzi unakwenda vizuri, “ingawa watu wachache wamejitokeza ila uchaguzi unakwenda vizuri.”

Katika Jiji la Arusha unafanyika uchaguzi katika kata nne baada ya waliokuwa madiwani wa Chadema kujiuzulu na kuhamia CCM ambako wamepitishwa kuwania tena nafasi hiyo kwa tiketi ya chama hicho tawala

Vurugu zaibuka Kwenye Marudio ya uchaguzi Mdogo Jijini Arusha, Polisi wachunguza Vurugu zaibuka Kwenye Marudio ya uchaguzi Mdogo Jijini Arusha, Polisi wachunguza Reviewed by KUSAGANEWS on August 12, 2018 Rating: 5

No comments: