Mtalii atafunwa na Kiboko wakati akitaka kumpiga Picha


Nakuru, Kenya. Mtalii kutoka China, Chang Ming Chuang amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kiboko nchini Kenya,.

Mtalii huyo mwenye umri wa miaka 66 amefariki baada ya kuvamiwa na kiboko alipokuwa akijaribu kumpiga picha

Taarifa kutoka Mamlaka ya hifadhi ya wanyama pori ya Kenya imeandika kwenye mtandao wake wa tweeter kuwa raia huyo kutoka China alivamiwa na kiboko wakati alipokuwa anampiga picha katika Ziwa Naivasha eneo la Sopa Resort Nakuru

Taarifa hiyo iliongeza kwamba mwenzake waliyekuwa wameongozana naye aliyefahamika kwa jina la Wu Peng Te mwenye umri wa miaka 62 alinusurika lakini bado yupo hospitali kwa ajili ya matibabu.

Ming Chuang alifariki alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali ya wilaya ya Naivasha

Wananchi wa eneo hilo walilalamika wakisema kwamba viboko hao huwavamia usiku kwani wakati huo macho yao huona zaidi kuliko mchana

Kwa mujibu wa mkazi wa kijiji, Safari Kadenge Karisa, alisema idadi ya viboko imeongezeka wengi wao ikifika usiku huvamia wenyeji kwenye makaazi yao

Alisema kwamba wanapotoa taarifa shirika la huduma la wanyama pori wanachelewa kufika kwa ajili ya kutoa msaada

Mtalii atafunwa na Kiboko wakati akitaka kumpiga Picha Mtalii atafunwa na Kiboko wakati akitaka kumpiga Picha Reviewed by KUSAGANEWS on August 12, 2018 Rating: 5

No comments: