Jeshi la Polisi mkoani Arusha
limesema limefungua jalada la uchunguzi la tukio la vurugu katika uchaguzi
mdogo wa marudio kata ya Kaloleni jijini Arusha baada ya watu wawili kudaiwa
kuchomwa visu na kikundi cha vijana wa 'Green guard' kutoka CCM.
Akizungumza na Kusaganews kwa
njia ya Simu Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi amesema walipigiwa simu na Mbunge wa Arusha wa
Mjini (CHADEMA), Godbless Lema kuwa mgombea wao Boniface Kimario amevamiwa na
kuamuru askari waliokuwa karibu na maeno hayo kuenda kutuliza hali ya usalama.
"Asubuhi kulitokea ushabiki wa
kisiasa kati ya makundi mawili ambayo ni ndio sasa hivi tunachunguza, na
ushabiki huo ndio ulisababisha huyo mgombea wa CHADEMA kupigana na watu
wengine. Kutokana na maelezo yake amesema akiwaona hao watu anawatambua hivyo
tunamsubiri amalize kutibiwa ili aje atuambie ni wakina nani hasa. Lakini yeye
hakuchomwa kisu", amesema
Kamanda Ng'azi.
Pamoja na hayo, Kamanda Ng'azi
ameendelea kwa kusema "isipokuwa kuna mwanachama mmoja wa CCM
alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali juu ya kiwiko chake cha mkono wake wa
kulia. Tumeshamkamata mtuhumiwa mmoja ambaye amemjeruhi mwanachama wa CCM"
Mbali na hilo, Kamanda Ng'azi
amesema hali ya uchaguzi inaendelea vizuri katika mkoani mzima wa Arusha hadi
hivi sasa ambao una jumla ya kata tatu ambazo ni Kaloleni, Daraja Mbili pamoja
na Osunyai
Mgombea wa CHADEMA ashambuliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment