Serikali ya awamu ya
tano iliyopo chini ya Rais Magufuli imefunguka na kukanusha taarifa za
kutelekeza mradi wa gesi asili kwenye kuzalisha umeme kama alivyodai Mbunge wa
Mtama, Nape Nnauye wakati alipokuwa anatoa maoni yake juu ya hotuba ya Waziri
Mkuu Kasim Majaliwa Bungeni.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo (Aprili 10, 2018) kwenye mkutano wa 11 kikao
cha sita kinachoendelea kufanyika mkoani Dodoma pindi alipokuwa anatoa maelezo
ya jumla kwa baadhi ya hoja zilizotolewa na Wabunge katika kikao cha Bunge cha
11 zilizoelekezwa katika Wizara yake hususan suala la vyanzo vya kuzalisha
umeme kwa upande wa gesi asilia pamoja na maji ambalo lilitajwa kwa kiasi
kikubwa na Mbunge Nape aliyedai serikali imewasaliti wananchi wa Mkoa wa Lindi
na Mtwara kutokana na kutoonekana neno gesi kwenye hotuba ya Waziri Mkuu yote.
"Nianze kuwatoa wasiwasi
wabunge, kwamba sio kweli kuwa vyanzo vya maji vinavyotumika kuzalisha umeme
havijatajwa katika Ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015 kama ilivyokuwa
imedaiwa hapo awali. Ilani imetaja vyanzo haijabainisha mradi kwa mradi. Katika
Ilani yetu ya CCM aya 43.a imeeleza vyanzo vya msingi ambavyo serikali
itavielekeza katika kuzalisha umeme wa uhakika na unaotabirika kwa gharama
nafuu na vyanzo vya maji vikiwemo", amesema
Dkt. Kalemani.
Pamoja na hayo, Dkt. Kalemani
ameendelea kwa kusema "ukienda kwenye mpango wa miaka wa miaka
5, ukurasa wa 81 umetaja bayana kadharika, vyanzo halali vitakavyotupungukia
bugudha, tofauti ndogo ndogo na migogoro ya upungufu ya umeme ikiwemo vyanzo
vya gesi ya asilia, maji, makaa ya mawe pamoja na upepo. Tunapotaja vyanzo vya
kuzalisha umeme kimsingi hatutaji mradi kwa mradi".
Dkt. Kelemani amesisitiza kuwa...
"Serikali haitaweza kutelekeza
kutumia gesi ya asilia hivi sasa tunayo Tilioni 57.5 ya gesi asilia na umeme
kwa kiasi kikubwa tunaotumia sasa hivi zaidi ya MW 787 zinatokana na gesi
asilia. Kwa hiyo sio kweli kwamba tumetelekeza matumuzi ya gesi asilia".
Kwa upande mwingine, Dkt. Kalemani
amesema bado matumizi ya gesi ya asili ni makubwa na serikali wapo makini nalo
kwa hilo sana.
SERIKALI YAKANUSHA TAARIFA YA NAPE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment