Rais John Magufuli ameukumbuka wimbo wa Ney
wa Mitego wa ‘Wapo’ ambao ulifungiwa na baadaye kuagiza ufunguliwe.
Tukio hilo limetokea leo Aprili 7, alipokuwa
akimaliza kuhutubia katika uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia
mjini Arusha kitakachosaidia kutoa huduma kwa watalii na maofisa wa kibalozi
Hafla hiyo imekwenda sambamba na uzinduzi wa
nyumba 31 za polisi, ambapo wageni mbalimbali walihudhuria wakiwemo wakuu wa
polisi wastaafu
Hata hivyo, katika kutaka kuwataja mmoja
mmoja waliohudhuria, Rais Magufuli alijikuta akitaja baadhi ya majina na
kuongeza neno yupo na baadaye kusema kuwa angekuwa msanii angeimba ule wimbo wa
‘Wapo’, maneno yaliyosababisha umati uliohudhuria shughuli hiyo kushangalia
Machi 26, mwaka jana wimbo huo wa Ney
ulifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), uliodaiwa kuwa ulimkashifu
Rais
Hata hivyo siku inayofuata, Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alitangaza
kuufungulia, agizo ambalo alidai limetoka kwa Rais
Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, Rais
alifurahishwa na ‘Wapo’ huku akimshauri mwanamuziki huo kutaja majina ya watu
wengine kwenye wimbo huo kama vile wakwepa kodi, wauza unga, wabwia unga na
watu wengine wasiokuwa na maadili
Mbali ya kufungiwa wimbo, pia Ney alijikuta
akikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mjini Morogoro ambapo nao waliamuriwa
kumwachia huru.
Raisi Magufuli aukumbuka wimbo wa ‘Wapo’ wa Ney
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment