RAISI MAGUFULI ATOA BILIONI 10 KWA AJILI YA ASKARI POLISI


Raisi Dokta John Magufuli ametoa shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari wenye vyeo vya chini ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi.

Amesema hayo jana wakati akihutubia katika ufunguzi wa nyumba za askari na maonyesho ya kazi za polisi ambapo amewataka wabunge wote nchini kusaidia kujenga nyumba za polisi kupitia fedha za jimbo kwani polisi wanaishi maisha yasiyo mazuri hivyo wanapaswa kutambua jukumu lao.

Aidha Dokta Magufuli ametangaza ajira 1500 kwa askari polisi waliotoka JKT ikiwa ni pamoja na kumtaka IGP Sirro kukaa na makamishna wa jeshi hilo ili kuangalia askari wanaostahili kupandishwa vyeo nay eye atapitisha.

Pia amewataka askari polisi kutokatishwa tama ya maneno ya kashfa na kebehi yanayosemwa dhidi yao kwani watanzania waliokuwa wengi wanatambua na kuthamini kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kulinda nchi.

Hata hivyo katika kuadhimisha siku ya Karume Raisi Magufuli amewataka watanzania kuyaenzi maisha ya hayati Amani Abeid Karume kwa kulinda Uhuru uliopo kudumisha amani pamoja na kuchapa kazi.

RAISI MAGUFULI ATOA BILIONI 10 KWA AJILI YA ASKARI POLISI RAISI MAGUFULI ATOA BILIONI 10  KWA AJILI YA ASKARI POLISI Reviewed by KUSAGANEWS on April 07, 2018 Rating: 5

No comments: