Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchini Urusi na Rwanda
kutumia fursa hiyo kwa kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuwavutia
wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii.
Ametoa maagizo hayo leo wakati
akizungumza na Balozi Ernest Mangu anayewakilisha Tanzania nchini Rwanda na
Balozi Simon Mumwi anayewakilisha Tazania nchini Urusi, katika ofisi ya Waziri
Mkuu mjini Dodoma.
Aidha amewataka Mabalozi kila mwisho
wa mwaka wajifanyie tathmini ya mafanikio waliyoyapata kutokana na
uwakilishi wao katika Mataifa ambayo ni kwa kiasi gani wamechangia kwenye
uboreshaji wa maendeleo ya Taifa.
Waziri Mkuu amesema Tanzania ina
vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na uwepo wa mbunga za wanyama, hivyo
ni vyema wanapoondoka wachukue nyaraka zote zitakazowasaidia katika kutangaza
vivutio vya utalii ili kuongeza idadi ya watalii nchini.
Amesema mbali na kutangaza sekta ya
utalii, pia watafute wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta nyingine
kama vile madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa
Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
“Pia mkajifunze mbinu ambazo
wenzetu wanazitumia katika kuboresha sekta mbalimbali ambazo na sisi tunazo
hapa nchini kama za viwanda na kisha mje mtueleze namna ya kuziboresha.
Kujifunza ni jambo zuri hivyo msisite kufanya hivyo huko muendako.”
Majaliwa.
Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi
hao wakawatambue na kuwaunganisha Watanzania waishio kwenye nchi wanazoiwakilisha
ili nao washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na wawasisitize wafuate sheria
za nchi wanazoishi na wakumbuke nyumbani.
Majaliwa awapa majukumu Mabalozi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment