MKUU wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki, amelazimika kuubeba
mzigo wa kulipa gharama za kujiunga na bima ya afya kwa watoto 16 wenye ulemavu
wa ngozi, baada ya kuelezwa hawana uwezo na wanyanyasika kupata huduma za afya.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwatembelea watoto hao ambao
wamechukuliwa na Shirika la Land Mark World Mission kwa ajili ya kusaidiwa
kupata huduma muhimu za kibindamu
“Najua kuna sera ya afya ya mwaka 2007 ambayo inaweza kulibeba
kundi hili la watu wenye ulemavu kupata msamaha,
lakini kwa sababu mpaka sasa hawajapata huo msamaha, mimi nawalipia watoto 16
ili waweze kufikia huduma za tiba katika hospitali zetu,” alisema.
Baada ya kuguswa na hali hiyo, baadhi ya wafanyabiashara na
wadau wengine wa maendeleo walilazimika kumuunga mkono Mkuu huyo wa wilaya na
kuwalipia Bima ya Afya iliyoboreshwa (iCHF), watoto wengine 23 wenye ulemavu na
hivyo kufikia idadi ya wanufaika 39.
Kwa mujibu wa Staki, katika kuweka uwiano sawa kwa Watanzania
wote bila ubaguzi, serikali ya awamu ya tano ina pendekezo la kutoa bima ya
afya ya lazima kwa watu wote ambao utasaidia pia kwa watu wenye msamaha kupata
huduma bora.
Hivi karibuni, serikali ilisema inafikiria kutoa huduma hiyo kwa
kundi la watu wasio na uwezo na wenye mahitaji maalumu wakiwamo wazee na wenye
ulemavu.
Hata hivyo, sera ya taifa ya afya imeainisha makundi maalumu
yanayostahili kupata msamaha wa huduma za afya katika vituo vyote vya kutolea
huduma kuwa ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 60, watoto chini ya miaka
mitano, waishio katika mazingira hatarishi, wajawazito na wasiojiweza kiuchumi.
DS SAME AKATIA WATOTO 16 WENYE ULEMAVU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment