Mwanaume mmoja amekutwa
na balaa la kutokwa na funza sehemu za siri, baada ya kuiba mke wa mtu ambaye
ni mke wa bosi wake, huko Kaunti ya Busia nchini Kenya.
Akizungumza kwa sauti ya kulia huku
akiomba msamaha, mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa, alisikika akimsihi
bosi wake aliyejulikana kwa jina la Mr. Ouma amsamehe kwa alichofanya na
kuapa kutorudia, huku akionyesha namna wadudu hao wanavyotoka kwenye sehemu
zake za siri.
“Mama nisaidie nakufa, nakubali
nimefanya, nisamehe ndugu yangu, siwezi rudia mara nyingine, ndugu yangu
nisaidie”, alisikika mwanaume huyo akimsihi bosi wake.
Kwa upande wa bosi wake huyo amesema
kuwa alimuajiri mwanaume huyo kufanya kibarua cha kupalilia shamba, lakini
alijiongeza na kujipa kibarua cha kulala na mke wake, na alishamuonya lakini
hakutaka kusikia na kuzidi kuendelea mpaka siku moja alimfuma kitandani kwake
akiwa na mkewe.
“Mimi nilienda safari lakini
nikaambiwa kuhusu wao, nikakaa kimya, siku moja nikamkuta kitandani kwangu na
mke wangu, mke wangu akaondoka kwenda naye kwake, yeye mwanaume akaniambia wewe
huwezi kazi ya nyumba, nikashtuka sana kuniambia hayo, nikipiga simu ya mke
wangu yeye ndio anapokea, nikaenda kwa mganga nikataka kuwapa fundisho”,
amesema Mr. Ouma ambaye mmiliki wa mke.
Baada ya tukio hilo Mr. Ouma alimleta
mganga ambaye alimfuata mara ya kwanza kumtibia mwizi huyo, na hatimaye
kupona na wadudu kuuacha kutoka, na kumuacha mke wake hapo hapo.
Atokwa funza sehemu za siri kwa kuiba mke wa mtu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment