Kaimu kamanda wa polisi kaanda maalum ya Dar es salaam Lucas Mkondya akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam siku ya leo limetoa taarifa ya matukio matatu tofauti likiwemo kukamata silaha moja aina ya shotgun,kuwakamata watuhumiwa wanne na magari mawili ya wizi pamoja na watuhumiwa 250 kwa makosa ya kihalifu na madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu kamanda wa polisi kaanda maalum ya Dar es salaam Lucas Mkondya amesema katika tukio la kwanza limetokea mnamo tar 16/7/2017 ambapo katika maeneo ya pemba mnazi kigamboni wamefanikiwa kukamata silaha moja aina ya Shotgun ikiwa na risasi tano ndani ya magazine.
Aidha amesema tukio lingine limetokea mnamo tar 14/7 katika maeneo ya mtaa wa uhuru na muheza Pilisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wakiwa na Televisheni flat scree,pamoja na simu 7 za wizi.
Kufuatia muendelezo wa mahojiano na watuhumiwa waliokamatwa jeshi la polisi limesema limefanikiwa kuwa kamata watuhumiwa wengine watatu wakiwa na magari ya wizi likiwemo gari lenye namba za usajili T 730 CTJ aina ya Toyota rav 4na lingine gari namba T.212 DEF Toyota IST ambayo iliibiwa mnamo may mosi mwaka huu huko kipunguni Moshi Bar.
Hata hivyo Jeshi la polisi limesema watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa kulingana na makosa yao ns pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria
No comments:
Post a Comment