Rais John Magufuli ameagiza kamanda
wa polisi wa Wilaya ya Sumbawanga, Polycarp Urio kusimamishwa kazi kwa
madai ya kushindwa kutekeleza maagizo aliyopewa na Waziri wa Mambo ya Ndani,
Kangi Lugola.
Agizo la Urio aliyekuwa akikaimu
nafasi ya kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa kusimamishwa kazi limetolewa leo
Jumapili Oktoba 6, 2019 baada ya Rais Magufuli kumpigia simu Inspekta Jenerali
wa Polisi (IGP), Simon Sirro na kumtaka kumsimamisha kazi Urio.
Septemba 30, 2019 alipewa maelekezo
ya kuwahamisha kazi askari tisa wa kituo cha polisi Laela kutokana na tuhuma za
uonevu na kuomba rushwa lakini hakufanya hivyo.
Leo akiwa kwenye uzinduzi wa
barabara ya Tunduma-Sumbawanga, Rais Magufuli alimuuliza kamanda wa
polisi wa mkoa huo, Mathias Nyange kuhusu askari hao ila alionyesha
kutofahamu chochote.
“Sina hayo majina na bahati mbaya
sifahamu chochote sikuwepo ofisini aliyekuwepo hakunipa taarifa yoyote kuhusu
maelekezo hayo,” amesema Kyando.
Baada ya majibu hayo Rais Magufuli
alimpigia simu IGP Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi Urio.
“Nataka umsimamishe kazi na umshushe
cheo maelekezo mengine nitakupa, anapewa maelekezo na waziri hataki
kutekeleza,” amesema Magufuli.
Magufuli amtaka IGP Sirro kumsimamisha kazi kigogo poli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment