Mahakama ya Wilaya ya Lindi, mkoani
Mtwara, imemuhukumu mkazi wa Mitema aliyefahamika kwa jina la Kijazi Ally (29),
kifungo cha miezi 36 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili,
likiwemo la kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,
mshtakiwa aliulizwa kama anazo sababu za msingi, zitakazoishawishi Mahakama
isimpe adhabu kali kwa makosa aliyokutwa nayo, ambapo katika kujitetea kwake
alikiri kosa hilo na kudai kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza na alilitenda
kwa sababu ya njaa na kuahidi kutorudia tena.
Baada ya utetezi huo, Hakimu Kiswaga
alimuuliza Mwanasheria wa Serikali Godfrey Mramba, kama ana kumbukumbu ya
makosa ya zamani kwa mshtakiwa,ambapo alijibu kuwa hana lakini aliomba apewe
adhabu kali, kwani ni mwizi mzoefu anayesumbua wakazi wa Mji wa Lindi.
Mramba alisema licha ya kutokuwa na
kumbukumbu kwa makosa ya zamani kwa mshtakiwa,lakini tayari anakabiliwa na kesi
nyingine inayohusu vitendo vya uvunjaji wa nyumba za watu nyakati za usiku na
ipo katika Mahakama hiyo.
Kufuatia kesi hiyo namba
14/2019, Hakimu Kiswaga alimhukumu mshtakiwa huyo kifungo cha miezi 36
Jela miaka 3, adai alifanya kosa sababu ya njaa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment