Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL),
imesitisha safari za ndege zake zinazofanya safari kuelekea Afrika Kusini,
kuanzia kesho Oktoba 7 na kuagiza abiria wote waliokuwa wamekata tiketi
kurudishiwa nauli zao.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi
wa ATCL Ladislaus Matindi, na kuagiza mawakala wote kurejesha nauli za abiria,
waliokuwa wamekwishakata tiketi kwa ajili ya safari na kwamba safari hizo
zimesimamishwa hadi taarifa kamili itakapotolewa tena.
Ikumbukwe kuwa hapo awali, Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, alitoa tamko rasmi la
kusitisha safari za ndege hizo kufuatia vuguvugu la machafuko lililokuwa
likiendelea Afrika Kusini, kati ya wazawa na raia wa mataifa mengine.
Mnamo Agosti 23, 2019,ndege ya ATCL
aina ya Bombadier Q220 - 300, ilishikiliwa nchini humo kwa amri ya mahakama ya
Guateng nchini humo, ambapo baadaye iliachiwa huru baada ya mawakili wa
Serikali kuishinda kesi dhidi ya mkulima.
ATCL yasitisha safari za Afrika Kusini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment