JESHI la polisi mkoani Pwani,
limekamata madumu 859 ya mafuta ya kula yanayodaiwa kutolipiwa ushuru ,yenye
thamani takriban milioni 50 ,huko Chemchem kata ya Magomeni ,Bagamoyo.
Akithibitisha kuhusu tukio hilo,
kamanda wa polisi mkoani hapo,Wankyo Nyigesa alisema ,madumu hayo yalikuwa
yakisafirishwa na Christopher Emmanuel (32).
Alieleza kuwa, Christopher
aliyasafirisha madumu hayo kupitia gari yake namba T.621 BCG aina ya fuso baada
ya kukwepa kulipa ushuru kwenye moja ya bandari bubu Bagamoyo.
“Tunachunguza risiti zake za malipo
kwani pia zina TIN namba tofauti,tunamshikilia mtu huyu pamoja na
aliyeshirikiana nae kutoa Hassan Saidi mpemba huyu mkazi wa Bagamoyo.”
Wankyo alisema, huo ni usafirishaji
haramu na kulitia hasara Taifa kwa kukwepa kulipa ushuru ama kodi,hivyo
aliwaasa wananchi kuacha biashara za magendo.
Kamanda huyo alifafanua,
wafanyabiashara wanapaswa kulipa ushuru kwa maendeleo ya Taifa na sio kutaka
faida kwa njia za mkato.
Alibainisha hawatawaachia nafasi
wakwepa ushuru na kudhibiti mianya ya kukwepa ushuru kwenye bandari zote bubu
kwakuwa zinafahamika.
Polisi pwani yakamata madumu 859 ya mafuta ya kula yasiolipiwa ushuru takriban mil.50
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 16, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment