Wakili
Jeremiah Mtobesya anayewatetea viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wa
chama hicho, Freeman Mbowe, amejitoa kwenye kesi hiyo
Mtobesya
amechukua uamuzi huo leo Agosti 23 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri
Wakili huyo
alijitoa kuwatetea washtakiwa hao mara baada ya Mahakama ya Hakimu Kisutu
kuyatupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka
huu iahirishwe katika Mahakama ya Kisutu ili kusubiri maombi yao na
rufaa yaliyopo Mahakama ya Rufani yasikilizwe na kutolewa maamuzi
Hata hivyo
Hakimu Mashauri aliyatupilia mbali maombi hayo kwa sababu kifungu cha sheria
walichotumia cha 225 (1) (2) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20
iliyofanyiwa marekebisho2002 hakiipi mamlaka hayo
Viongozi hao
tisa wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo kuhamasisha maandamano Februari
16 mwaka huu siku moja ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni
Wakili ajitoa kesi ya kina Mbowe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment