Waandishi wa habari za jinsia kupewa tuzo kesho


Waandishi wa habari za jinsia nchini kesho watakabidhiwa tuzo, katika kinyang'anyoro kilichoshirikisha vyombo vya habari 15, vilivyo kubaliana kuandika habari kwa mlengo wa kijinsia

Waandishi hao watapewa tuzo hizo katika mkutano wa Jinsia na Habari ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kitengo cha Wanawake (UN Women), unaoendelea jijini Dar es Salaam

Akizungumza leo Agosti 23, Mmoja wa Waratibu wa mkutano huo na mtafiti kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) Gladness Munuo amesema tuzo hizo zinashindaniwa katika vipengere vitatu vya  luninga, magazeti na redio

"Tulikubaliana na vyombo vya habari juu ya kuripoti kwa mlengo wa kijinsia, kwa maana ya kwamba hata wanapohojiwa watu watano basi miongoni mwao wawepo wanawake," amesema

Munuo amesema bado suala la jinsia linahitaji msukumo hasa wanawake ambao wengi wao hawapewi nafasi na hata wakuzungumziwa ni mwa mlengo hasi na sio chanya

"Kwa hiyo hizi tuzo zitatoa msukumo kwa vyombo vyetu na wanahabari kuona suala la jinsia ni la muhimu,"amesema

Waandishi wa habari za jinsia kupewa tuzo kesho Waandishi wa habari za jinsia kupewa tuzo kesho Reviewed by KUSAGANEWS on August 23, 2018 Rating: 5

No comments: