Baada ya
Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kufutiwa
mashtaka na kukamatwa tena hatimaye amesomewa mashtaka yab uhaini
Wine
alikamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya
umiliki haramu wa silaha nchini humo
Muda mfupi
baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na kushtakiwa katika
mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine
waliokamatwa
Mbunge huyo
ambaye pia ni mwanamuziki kwa jina maarufu Bobi Wine leo
alifikishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda
akitumia usafiri wa helkopta
Mawakili wake
awali waliambiwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye
anakoshikiliwa mjini Kampala
Kumekuwa na
shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru
Bobi Wine asomewa mashtaka ya uhaini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment